You are: Home > About Us

ABOUT US

Kuanzisha kwa Benk ya Kiislamu ya PBZ kunatokana na maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzbiar katika mwaka 2007, baada ya kufanyika utafiti (survey) ambayo ilibaini kuwa wananchi wengi hawaweki fedha zao benki kutokana na imani za dini zao ambazo zinakataza riba.

Ili benki kwenda sambamba na mahitaji ya wateje wake, Benki katika tarehe 17 Januari 2011 ilifungua tawi la kwanza la Benki ya Kiislamu ya PBZ katika jingo la ZSSF, Mwanakwerekwe Zanzibar. Benki ya Kiislamu ya PBZ ilianza kutoa huduma rasimi katika mwezi wa Jarunary 2011 katika tawi la Mwanakwerekwe, Zanzibar.
Benki iliendela kufungua matawi mengine mawili katika mwaka 2011. Tawi moja lipo Kariakoo, Dar es Salaaam katika mtaa wa Lumbua/Mahiwa na tawi la pili lipo Chake Chake, Pemba katika mtaa wa Tibirizi/Wawi.

Benki ya Kiislamu ya PBZ inaamini kuwa huduma inazotoa ambazo zinaenda na misingi ya Sharia ya Kiislamu ni kwa ajili ya watu wote waislamu na wasiokua waislamu. Hali hii inapelekea kuendelea kuanzishwa kwa huduma nyingine zenye kuleta ushindani wa kutoa huduma bora kwa wananchi. Benki ya Kiislamu ya PBZ inasaidia katika kujenga na kukuza maadili ya jamii, kukuza ushirikiano wa jamii, na kujenga utawala bora kwa kutoa huduma bila kujali itikadi/imani za kidini. Kwa sasa Benki ya Kiislamu ya PBZ ina matawi matatu katika maeneo ya Unguja, Pemba na Dar es Salaam.

Dira

Kuwa na taasisi ya fedha inayotoa huduma bora za benki zinazofuata misingi ya Sharia na kuisaidia Serikali katika kukuza uchumi, ustawi wa jamii na kupunguza umaskini.

Dhamira yetu

Kutoa huduma za benki zenye kufuata misingi ya Shariah kwa bei nafuu. Ili kutekeleza hilo, Benki itatoa huduma mbalimbali kulingana na mahitaji halisi ya wateja kwa kutumia Teknohama na kuwezesha mmiliki, mteja na wafanyakazi kupata faida au kipato halali na kuisaidia Serikali katika kukuza Uchumi na kupunguza Umaskini.

Maadili yetu

Haki, Uadilifu, Kuzingatia Utaalamu, Uaminifu na uwajibikaji katika kutunza amana na kutoa huduma.

 

 

 

PBZ ISLAMIC BANKING
 
TUKO MTWARA